Sera ya kurudisha pesa
Tunataka uridhike na unachonunua. Ukurasa huu unaeleza lini unaweza kurudishiwa pesa zako.
Imesasishwa mwisho: 7 Oktoba 2026
Hosting na VPS
Usiporidhika na mpango mpya wa hosting au VPS, tuambie ndani ya siku 7 tangu malipo yako ya kwanza na tutakurudishia malipo hayo yote.
Baada ya siku 7 haturudishi malipo ya kipindi cha sasa, lakini unaweza kusitisha kabla ya kuhuisha ili usitozwe tena.
2. Domain
Usajili na uhuishaji wa domain hairudishwi baada ya domain kusajiliwa, kwa sababu ada hulipwa kwa msajili mkuu.
3. Tovuti, chapa, video na upigaji picha
Hii ni miradi maalum. Ikiwa kianzio kimelipwa na hatujaanza, tunakirudisha. Kazi ikishaanza, kianzio kinagharamia kazi iliyofanyika hadi sasa.
Tusipokabidhi kilichoelezwa kwenye ofa ya bei, tutarekebisha bila gharama. Tusipoweza, tutarudisha malipo ya sehemu ambayo haikukabidhiwa.
4. Hali nyingine
Pesa hazirudishwi kwa matatizo yaliyosababishwa na mabadiliko uliyofanya, huduma za watu wengine, au huduma zilizosimamishwa kwa sababu masharti haya yalivunjwa.
5. Jinsi ya kuomba
Tuandikie kwa WhatsApp au kupitia shaiyache@gmail.com ukitaja jina lako na ulichonunua. Marejesho yaliyoidhinishwa hulipwa kwa njia ile ile uliyolipia, kwa kawaida ndani ya siku 10 za kazi.